Afya

Taasisi ya utafiti ya ugonjwa wa saratani Uingereza yaeleza, Unene unasabisha saratani kuliko uvutaji sigara kwa watu wengi, fahamu zaidi

Taasisi ya utafiti ya ugonjwa wa saratani Uingereza yaeleza, Unene unasabisha saratani kuliko uvutaji sigara kwa watu wengi, fahamu zaidi

Unene kwa sasa umekuwa moja ya kisababishi cha ugonjwa wa saratani nchini Uingereza kuliko uvutaji sigara, taasisi ya saratani nchini humo imeeleza. Taasisi ya utafiti ya ugonjwa wa saratani imesema, saratani ya ini, utumbo, ovari zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na uzito mkubwa kuliko kuvuta tumbaku.

Inasema mamilioni wako hatarini kuugua saratani kwasababu ya uzito na kuwa watu wenye uzito mkubwa huzidi idadi ya wavuta sigara kwa wastani wa watu wawili kwa mmoja.

Lakini matangazo ya mabango ya kampeni kuhusu unene na hatari ya kupata saratani yamekosolewa kwa kujeli watu wanene.

Maangazo ya tahadhari kuhusu saratani

Kwa mujibu wa BBC. Si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kushutumiwa kukejeli watu wanene. Wengine wakisema kuweka tangazo hilo kama vile matangazo ya pakiti za sigara si jambo zuri.

https://twitter.com/KenLynch73/status/1144936624742195200?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1144936624742195200&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.bbc.com%2Fswahili%2Fhabari-48865706

Lakini taasisi hiyo imejitetea kuwa haiwalaumu watu walio na uzito mkubwa.

Wala haisemi kuwa uvutaji wa sigara ni sawa na kuwa na uzito mkubwa wakihusisha na hatari ya kupata saratani. Vyote viwili vinahatarisha afya.

Lakini taasisi hiyo imesema uzito mkubwa au unene husababisha wagonjwa wa saratani 22,800 kila mwaka, ukilinganisha na uvutaji wa sigara unasababisha watu 54,300 kuugua saratani.

Lakini wakati idadi ya wavuta sigara ikipungua, idadi ya watu wenye uzito mkubwa inaongezeka, suala la kushughulikiwa.

Wakati uhusiano kati ya uzito mkubwa na saratani ukibainishwa vyema, kibaiolojia bado haijaeleweka vyema

Kuwa na uzito mkubwa au mnene haimaanishi kuwa lazima mtu huyo apate saratani, lakini mtu huyo anaongeza hatari ya kupata ugonjwa huo.

Ongezeko la hatari hujitokeza zaidi iwapo mtu ataongezeka uzito zaidi.

Kwa mujibu wa watafiti saratani mbalimbali zinahusishwa na uzito mkubwa: Saratani ya matiti kwa wanawake waliokoma hedhi (menopause), utumbo, ini, saratani ya damu, saratani ya ubongo, koo, tezi, figo, kongosho, tumbo,ovari. Uhusiano kati ya unene na saratani ni kwa watu wakubwa pekee, ingawa kwa watoto wadogo ni muhimu kuwa kwenye tahadhari pia.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents