Habari

Taasisi zinazohamasisha ushoga kufutwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametaka apewe taarifa kuhusu taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) wanaohamasisha au kutangaza ndoa za jinsia moja nchini ili azifutie usajili mara moja.

Waziri Nchemba aliyasema hayo Jumatatu hii mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na taasisi za Kijeshi za mkoa huo zikiwemo Uhamiaji, Polisi, Magereza na Zimamoto.

“Leteni majina ya taasisi hizo ili tuzifute kwani hazistahili kuendelea kufanya jambo hilo ambalo ni laana na halipaswi kufumbiwa macho ndani ya jamii,” alisema Nchemba.

Aidha Nchemba alisema kuwa taasisi hizo hazifai kwani zinafanya kazi ya laana ambayo ni kinyume cha maadili ya Kitanzania na hazistahili kuendelea kufanya kazi kwa upotoshaji huo. Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Bonaventura Mushongi alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi, ikiwa ni pamoja na magari.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents