Tupo Nawe

TAFITI: DAR kinara mikoa mitano Tanzania yenye watu wengi wenye magonjwa ya akili

Mkoa wa Dar es salaam umetajwa kuongoza kuwa na watu wengi wenye magonjwa ya akili ikiwa mbele ya mikoa mitano yenye watu wengi wenye magonjwa ya akili Tanzania.

Imeelezwa kuwa sababu za kimazingira ikiwemo ugumu wa maisha na matumizi ya vilevi, Ndio chanzo kikubwa cha tatizo hilo mijini kuliko vijijini.

Akizungumza na gazeti la Nipashe jana Oktoba 9, 2019, Daktari wa Afya ya Akili katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Omary Ububuyu, Amesema takwimu zilizopo kwa miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2018 zinaonyesha  magonjwa ya akili yameongezeka kutoka 301,000 hadi  356,000.

Kwa mwaka 2016 kulikuwa na wagonjwa 301,000 wanahusisha na magonjwa ya akili, kifafa na matumizi ya kilevi,” alisema wakati akizungumzia  maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani leo.

Ameeleza kuwa magonjwa ya kifafa kwa ujumla wake baadhi yametibiwa kwenye idara ya magonjwa ya akili na mengine nje ya idara ambapo yana takribani asilimia 50 ya wagonjwa wote. “Sasa magonjwa haya matatu katika takwimu za Wizara ya Afya na Tamisemi zinaonyesha katika vituo vya afya takribani wagonjwa 356,000 kwa mwaka 2018, pia asilimia 50 ya magonjwa ni ya akili na nyingine ni kifafa,” alisema na kuongeza:

Hii ni kwa hospitali ya mkoa na vituo vya afya, hapa hatujahusisha takwimu kutoka hospitali kama Muhimbili na Mirembe na hospitali zingine kubwa.“.

Akitaja mikoa inayoongoza, Dkt. Ububuyu Dk. Ububuyu amesema mijini kuna wagonjwa wengi zaidi ambapo takwimu hizo zinaonyesha Dar es Salaam inaongoza kuwa na wagonjwa asilimia 20 bila kujumuisha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mkoa mwingine ni Kilimanjaro, Tanga, Morogoro na Mwanza,  yote mitano ipo juu na hali hii hapo katika magonjwa ya akili peke yake hata magonjwa yasiyo ya kuambukiza hali ipo hivyo hivyo.“amesema Dkt. Ububuyu.

“Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza halafu mikoa mingine inafuata, Dar es Salaam ina asilimia 20, Kilimanjaro 9, na mingine asilimia 7 hadi 5. Mikoa yenye wagonjwa kidogo ni Katavi 0.1, Rukwa 4, Songwe pia ina asilimia chache ya wagonjwa,” amesema Dkt. Ububuyu.

Hata hivyo, alisema hali za kimazingira na vilevi ndizo zinazochangia zaidi kuliko viashiria vya kibaiolojia kwenye maeneo ya mijini kuliko vijijini.

Kuna vihatarishi vinavyosababisha magonjwa ya akili ambapo kikubwa namba moja ni vinasaba, vitu vya kibaiolojia kuna kupata majeraha ambayo yanaathiri ubongo, baadhi ya magonjwa yanayopanda kichwani ikiwamo malaria, HIV. “Pia matumizi ya vilevi kama pombe, bangi, sigara na vilevi vingine kwa kuwa vilevi kazi yake kubwa ni kushusha uwezo wa ubongo kufanya kazi na mambo yaliyokuwa yakitarajiwa,”amesema Dkt. Ububuyu.

Mtaalamu huyo alisema: “Utakuta vilevi vingi vinaweza kuwa vihatarishi, unaweza ukatumia bangi ukaumwa, pia hali ya kijamii yaani ya kiuchumi ikiwamo ugumu wa maisha yaani kuwa na hali ngumu kupita kiasi ambayo mtu hawezi kuimudu kama kufiwa mtu akashindwa kustahimilivu maumivu ya kupoteza kitu anachokipenda kama kazi, mwenza, rafiki au ndugu.

 

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW