Habari

Tahadhari yatolewa kwa wananchi juu ya ugonjwa hatari wa Chikungunya

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa ya Chikungunya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea Mombasa nchini Kenya.

Ummy Mwalimu

Taarifa hiyo iliyotolewa leo Ijumaa Januari 19, 2018 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu imesema kuwa mpaka sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) bado halijatoa taarifa rasmi lakini wao wanaotoa tahadhari kuzingatia muingiliano mkubwa wa watu baina ya nchini hizi mbili Kenya na Tanzania.

Wizara ya Afya imesema kuwa ugonjwa wa Chikungunya unasababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes na kusema ugonjwa huu si mgeni nchini Tanzania kwani ulishawahi kutokea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents