Bongo5 MakalaBurudani

Tahariri: Kwa uamuzi huu, wasanii wote wa Tanzania wanapaswa kuiga mfano wa Cpwaa

Cpwaa kupitia label yake ya muziki, Brainstorm Music, amepanga kuanzisha utaratibu ambao ulipaswa kuwa unafanywa na wasanii wote wa Tanzania hasa wale ambao wamekuwa wakifanya show nyingi kwa mwaka.

cpwaa1

Rapper huyo amesema ataanzisha utaratibu wa kuwalipa watayarishaji muziki fedha zinazotokana na matumizi ya nyimbo walizomtengenezea yeye ama wasanii watakaokuwa chini ya label hiyo. Huu ni utaratibu mpya kabisa kwa Tanzania, lakini kwa nchi zilizoendelea kama Marekani na kwingine, umekuwa ukifanyika kwa miaka mingi.

Katika utaratibu huu, wanamuziki hutakiwa huwalipa watayarishaji wa muziki asilimia kadhaa za fedha wanazoziingiza kutokana na matumizi ya nyimbo zao. Hapo, waandishi wa nyimbo nao pia hunufaika na gawio hilo. Kwa Tanzania, mtayarishaji anapolipwa gharama ya wimbo aliotengeneza, hicho ndio kipato cha mwisho anachokipata hata kama wimbo huo utamuingizia msanii mamilioni ya shilingi.

Mfano, mwaka jana Madee alidai kuwa wimbo wake ‘Sio Mimi’, ulimuuingizia si chini ya shilingi milioni 150 ambazo zilikuwa ni mali yake. Kwa utaratibu halali wa biashara ya muziki, Madee alitakiwa kutoa asilimia kadhaa ya fedha hizi kumpa producer wa wimbo huo, Zachaa/Marco Chali wa MJ Records hata kama alililipa fedha za kurekodi wimbo huo.

Kutokuwepo kwa utaratibu huo ndio maana kumefanya watayarishaji wengi wa muziki kuwa na maisha ya hali ya chini huku wasanii wanaowatengenezea nyimbo hizo wakipata mashavu mengi na kuishi maisha ya kifahari. Kinachoumiza zaidi ni kuwa gharama za kurekodi nyimbo Tanzania bado ziko chini. Gharama kubwa zaidi ya kurekodi wimbo kwenye studio maarufu ni takriban shilingi laki 5. Inaingiaje akilini kwa producer kuambulia shilingi laki 5 katika wimbo ambao msanii humuingizia mamilioni ya shilingi?

Watayarishaji wa muziki mara nyingi hukesha studio kutengeneza nyimbo, lakini malipo yao ni kidogo mno na hivyo kuna umuhimu mkubwa wa wao kuanza kupigania haki yao kupata royalties au gawio linalotokana na utumikaji wa nyimbo walizozitengeneza.

Hivyo tunampongeza sana Cpwaa kuwa kuchukuaa uamuzi huu ambao unatakiwa pia kuigwa na wasanii wengine.

“Kupitia Brainstormusic nimejifunza vitu vingi sana kuhusu sanaa ya muziki baadaa kufanya kazi na makampuni ya hapa Tanzania na nje.Nimesafiri nchi nyingi Africa na Asia kupitia muziki na kusema ukweli Tanzania kuna mambo mengi sana bado hayako sawa kwenye biashara ya muziki. Umefika muda wa sasa kushare experience na knowledge na kama tukifata utaratibu huu hakuna mtu atadhulumiwa wala kulalamika.Kila mdauanahusika,” amesema Cpwaa kwenye maelezo yake.

“Kwenye utayarishaji wa muziki kila mhusika huwa anakuwa kiwango fulani cha asilimia ya mapato anapata kutokana na mchango wake.Kwa kawaida mapato ya muziki “Royalties” hugawanywa kati ya Songwriter ( mtunzi wa nyimbo ambae ndio mmliki halali wa nyimbo), Producer ( Mtayarishaji), Performing Artist ( Muimbaji wa nyimbo) na Publisher au Record label ( wasambazaji na wasimamizi). Mgawanyo unatokana na kiwango cha mchango wa kila muhusika na mara nyingi huwa makubaliano kati ya wahusika. Kimataifa au kawaida mtunzi huchukua asilimia kubwa na wengine hupata sehemu tu mirabaha itakayokusanywa.

Kuanzia mwaka huu producer yeyote atakayefanya kazi na CPwaa chini ya usimamizi wa “Brainstormusic” basi atafaidika si tu kwenye malipo ya awali ya utengenezaji wa beat na studio time ila pia asilimia fulani ya mapatao ya mirabaha itakayoingizwa na kazi hiyo. Kimataifa producer huchukua kati ya 20 – 25% kutokana na kwamba yeye kama mtengenezaji wa beat basi ndio mmiliki wa ile beat. Huu ni utaratibu mpya utakuwepo kwa maproducer wote watakaofanya kazi na CPwaa au Brainstormusic kuanzia mwaka huu:

1.Kazi zote zitaandaliwa na kufanywa chini ya makubaliano yaliyoandikwa na kusainiwa na pande zote.Invoice na risiti zitahusika.

2.Brainstormusic ikinunua beat pamoja na haki miliki zake ( yaani producer akiuza beat jumla) basi hatapata share za mirabaha.

3.Kama Brainstormusic au Msanii wake atahusika kwenye hatua za utayarishaji beat,vionjo,idea,upangiliaji basi asilimia fulani ( chini ya makubaliano) ya mirabaa itatolewa na Brainstormusic kwa producer wa kazi hiyo.

4.Kama producer atahusika mwanzo mwisho kutengeneza na kukamilisha beat hiyo bila uhusika wa Brainstormusic au msanii wake basi producer atapata asilimia fulani kubwa zaidi ( chini ya makubaliano) ya mapato ya mirabaha ya kazi hiyo.

5. Ukiacha mapato ya mirabaha Brainstormusic itamlipa Producer au Studio gharama za kawaida ( Delivery / Studio Fee) kama utaratibu ulivyo sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents