Michezo

Taifa Queens kuchuana Singapore

Timu ya taifa ya netiboli Taifa Queens

 

Timu ya taifa ya netiboli Taifa Queens ya mpira wa mikono imeondoka nchini kwenda nchini Singapore kushiriki mashindano ya kimataifa, yanayoshirikisha mataifa sita ikiwemo Tanzania.

Timu hiyo ilikabidhiwa Bendera ya Taifa, kwenye kambi yao iliyo katika Shule ya Filbert Bayi, Mkuza Kibaha, na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Iddi Kipingu.

Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi, alitoa pongezi kwa wadau mbalimbali zikiwemo taasisi mbalimbali, Ikulu, Jeshi la Wananchi pamoja na Magereza kwa kuwagharamia wachezaji hao.

Baadhi ya wachezaji waliondoka ni pamoja na Nahodha Jackline Sikozi, Lilian Sylidion, Irene Elias, Lydia Samwel, Restituta Boniphace, Eva Peter, Veronica Kubiru, Sekela Dominick, Mwanaidi Hassan, Paskalia Kibayasa na Zuhura Twalibu.

Kwa upande wa Viongozi ni pamoja na Rose Kisiwa, kocha Simone Mckinns na msaidizi wake, Damian Chonya, ambaye pia ni mwamuzi wa kimataifa anayetambuliwa na IFNA na Daktari Richard Yomba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents