Michezo

Taifa Stars imeshindwa kutamba mbele ya Malawi

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Malawi katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya ‘FIFA’ mchezo uliyochezwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Malawi ilipata bao la mapema dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Robert Ngambi.

Stars ambao walikuwa wenyeji katika mchezo huo ilirejesha bao hilo kupitia kwa mchezaji wake anaekipiga  Difaa el Jadidi ya nchini Morocco, Simo Msuva dakika ya 57 kupitia mpira wa kona uliyokwenda moja kwa moja hadi nyavuni.

Mpaka mpira unamaliziki katika mchezo huo wa kirafiki Taifa Stars dhidi ya Malawi mabao ni 1-1.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents