Michezo

Taifa Stars itacheza hivi robo fainali Afrika Kusini kesho

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho Julai 2 itakuwa na kibarua kizito mbele ya Afrika Kusini kunakomichuano ya COSAFA inayo endelea huko nchini Afrika Kusini.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiingia uwanjani

 

Stars itacheza mchezo huo wa robo fainali dhidi ya mwenyeji Afrika Kusini baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Mauritius katika mchezo wake wa mwisho wa makundi.

Bao pekee la Stars lilifungwa na mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simon Msuva na kuiwezesha Tanzania kutinga hatua hiyo ya robo fainali ambapo Stars ni mgeni mualikwa kwakua hayupo katika ukanda wa COSAFA bali yupo katika Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents