Michezo

Taifa Stars kulipiza Kisasi Leo

Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, leo inacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu ya taifa ya Msumbiji, The Mambas, kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, leo inacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu ya taifa ya Msumbiji, The Mambas, kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Awali Stars ilipanga leo kucheza na timu ya taifa ya Misri, Pharaos, lakini mchezo huo umesogezwa mbele na Chama cha Soka cha Misri, EFA, mpaka Januari mwakani.

Stars ikiwa chini ya Marcio Maximo iliingia kambini siku sita zilizopita kujiandaa na mchezo huo na kocha huyo alisema kuwa mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na Msumbiji kuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu ambao wanacheza soka la kulipwa nchi za Ulaya.

Maximo alisema kuwa mechi hiyo itakuwa ni kipimo kizuri cha timu yake dhidi ya mechi inayofuata dhidi ya timu ya taifa ya Sudan na endapo wataibuka na ushindi itawaongezea morali katika mchezo huo unaofuata na wa marudiano.

Alisema wachezaji wake wote wako katika hali nzuri kuwakabili wapinzani hao na hana majeruhi hata mmoja.

“Naahidi kuwa wachezaji wangu wataonyesha kandanda safi ambalo ndio lina nafasi ya kuweza kuwapatia ushindi,“ alisema Maximo.

Akizungumza na Bongo5 leo, nahodha wa Stars, Henry Joseph alisema kuwa lengo ni kushinda na kulipiza kisasi kutokana na kufungwa na timu hiyo mwaka jana katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizopita.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents