Michezo

Taifa Stars yaiangusha Tanzania na Rais Magufuli nchini Lesotho kwa kukubali kichapo

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania, Taifa Stars imekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Lesotho kwenye mchezo wa kufuzu AFCON 2019.

Image result for taifa stars

Kwa matokeo hayo Taifa Stars inakuwa na alama 5 ikiwa imecheza michezo mitano jambo ambalo itahitajika kushinda dhidi ya Uganda kwenye mchezo wake wa mwisho huku ikiwaombea  Cape Verde wenye alama 4 waitandike Lesotho.

Bado matumaini ni madogo kwa Taifa Stars kufuzu kwenda AFCON 2019. Mapema kabla ya mchezo huo Rais Magufuli aliwaomba vijana hao warudi nchini na ushindi lakini ndio hivyo mpaka dakika 90 wamekubali kichapo.

Kwa upande mwingine, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kabla ya mchezo huo alisema kuwa endapo Taifa Stars itafungwa basi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe ni vyema akajiuzulu.

https://twitter.com/zittokabwe/status/1064173327906979840

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents