Michezo

Taifa Stars yaoga mvua ya magoli Algeria

Timu ya Taifa Stars imekubali kipigo cha magoli 4 kwa moja dhidi ya timu ya taifa yaAlgeria. Mechi hiyo imepigwa usiku wa kuamkia Ijumaa hii katika Uwanja wa Mustapha Tchaker huko Blida nchini humo.

Mabao ya Algeria katika mchezo huo ambao waliutawala kwa asilimia kubwa, yalifungwa na Baghdad Bounedjah kwenye dakika za 13 na 80, Shomari Kapombe akijifunga kwa kichwa dakika ya 43 na bao la mwisho likifungwa na Carl Medjan (52′).

Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva kufuatia kona safi ya Shiza Kichuya mnamo dakika ya 20.

Matokeo hayo yanaleta taswira mbovu kwa Tanzania haswa kuelekea kupanda kwa ubora wa viwango vya soka duniani.

Kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Stars itakuwa ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki, dhidi ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mechi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam, Machi 27 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents