Michezo

Taifa Stars yapata mualiko wa balozi kabla ya kuivaa Algeria usiku wa leo

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) hii leo majira ya saa 2: 00 usiku inatarajia kushuka uwanjani kuivaa Algeria kwenye mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA.

Kikosi cha Taifa Stars na viongozi wake hapo jana wamepata nafasi ya kualikwa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Omar Yusuph Mzee na kuandaliwa chakula cha usiku.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 – 27, 2018 dhidi ya timu za Taifa za Algeria na DR Congo.

Baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Stars itarejea nyumbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents