Michezo

Taifa Stars yashusha kipigo kikali kwa Botswana (Video)

Timu ya taifa ya Tanzania imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika ratiba ya FIFA uliyopigwa katika uwanja wa Uhuru na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harisson Mwakyembe na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Bao la kwanza la Simon Msuva

https://www.facebook.com/azamtvtz/videos/903983526434556/

Mabao ya Stars yakifungwa na kiungo wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga nchini Morocco katika Klabu ya Difaa El Jadidi inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo Simon Msuva.

Saimon Happygod Msuva ameipatia Stars mabao katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza na kipindi cha pili katika dakika ya 60 huku akionekana kufanya vizuri zaidi katika mchezo huo.

Bao la Pili la Simon Msuva katika kipindi cha pili

https://www.facebook.com/azamtvtz/videos/904023859763856/

Katika kikosi hicho cha kocha Salum Shabani Mayanga, kimefanya mabadiliko kadhaa wakati wa mchezo huo kwa kumtoa Mzamiru Yasin na kuingia, Raphael Daudi katika kipindi cha pili na kutoka Shiza Ramadhani Kichuya na nafasi yake kuchukuliwa na Faridi Musa,  Himid Mau akitoka na kuingia Said Hamisi Ndemla pia mfungaji wa mchezo huo Simon Msuva ikitoka na Mbwana Samatta akitoka pia.

Hizi ndizo takwimu za kipindi cha kwanza, Botswana wameongoza kwa umiliki wa mpira.

TAKWIMU: Hizi ndizo takwimu za mchezo baada ya kipindi cha pili: Tanzania 2-0 Botswana (Msuva 5′, 61)

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents