Tupo Nawe

Tajiri, Moise Katumbi aweka Bilioni 1 mezani, aituma TP Mazembe kufanya kazi moja tu kwa Simba

Mmiliki na mwenyekiti wa timu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo Moise Katumbi ameweka mezani bilioni moja kwaajili ya wachezaji na benchi la ufundi kuhakikisha wanaibuka na ushindi hii leo dhidi ya Simba SC.

Mabingwa hao mara tano wa klabu bingwa barani Afrika CAF, hapo baadae kidogo wanatarajia kushuka uwanjani huko Lubumbashi kiuwakabili Simba kwenye mchezo wa marudiano hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa.

Katika mchezo wa kwanza uliyopigwa hapa nyumbani Tanzania Simba SC ilitoka sare tasa ya bila kufungana dhidi ya Mazembe na hivyo kila mmoja bado ananafasi kubwa ya kusonga hatua inayofuata.

Mlezi huyo wa TP Mazembe, Katumbi ameweka kitita hicho cha fedha ili kuhakikisha vijana wake wanapata morali uwanjani na kuhakikisha wanatinga hatua ya nusu fainali hii ni kutokana na msimu uliyopita kutolewa kwenye hatua hiyo ya robo fainali.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW