Habari

Tajiri wa 107 wa Marekani ‘Paul Tudor Jones’ ndiye mwenyeji wa Oprah Winfrey aliyetua Serengeti

Tajiri namba 107 nchini Marekani (kwa mujibu wa Forbes), Paul Tudor Jones II, mwanzilishi wa kampuni ya Tudor Investment Corporation ndiye mwenyeji wa Malkia wa Talk Shows duniani, Oprah Winfrey aliyekuja Tanzania na kufikia mbugani, Serengeti.

ptj_4
Paul Tudor Jones

Oprah aliyetua Serengeti weekend hii alikuwa anatokea nchini Hispania na amekuja Tanzania kwa ziara binafsi. Alipokelewa na naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Oprah Winfrey Network 2011 Winter TCA Reception
Oprah Winfrey

Jones ambaye ana utajiri ufikao dola bilioni 3.3 ambao unamfanya pia awe tajiri wa 330 duniani, ni mwekezaji mkubwa huko Serengeti. Tajiri huyo ndiye mmiliki wa hoteli za kifahari mbugani huko za Singita Grumeti Reserves (SGR) ambazo zinajumuisha hoteli za , Sasakwa, Farufaru, Sabora Tented Camp na Singita Explore Mobile Camp.

Singita-Grumeti-Reserves-1
Serengeti Grumeti Reserves

Kwa mujibu wa jarida la Travel- Leisure la Marekani, hoteli hizo zinakamata nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfululizo kati ya hoteli 100 bora duniani.

Tudor Jones anamiliki acre 340,000 kwenye mbuga hiyo ya wanyama ya Serengeti. Tajiri huyo ndiye aliyedhamini ujenzi wa uwanja wa ndege uliopo Mugumu, Serengeti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents