Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Take Care ya Drake yatikisa chati za Billboard

Je unaweza kuuzuia mwanga gizani? Basi kama utaweza hilo itakuwa ni rahisi kusimamisha makali ya rapper Drake kwenye muziki.

Japo ameonekana kuwa kimpya kwa siku za hivi karibuni lakini Drake ameendelea kutikisa chati za Billboard kupitia albamu yake ya ‘Take Care’ aliyoiachia mwaka 2011.

‘Take Care’ imefanikiwa kushika nafasi ya 105 katika wiki yake ya 251 katika chati hizo. Albamu hiyo ina nyimbo 18 huku akiwakutanisha wasanii wengine kama Rihanna, The Weeknd, Nicki Minaj, Rick Ross, Lil Wayne, Birdman, Kendrick Lamar na wengine.

Albamu nyingine za msanii huyhuyo ambazo zimefanya vizuri ni ‘More Life’ ambayo imekaa kwenye chati hizo kwa wiki 40 na ‘Views’ ambayo ina wiki 86.

Kwa sasa rapper huyo ameonekana kuandaa albamu yake mpya ambapo mwezi August mwkaa huu alionekana akiwa karibu mjini Toronto na watayarishaji wa muziki kama London On Da Track na Pi’erre Bourne.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW