Habari

TAKUKURU kuwaburuza Mahakamani wanaodaiwa kutafuna Bilioni 2

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iko katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni mbili zinazowakabili viongozi wa kiwanda cha kukoboa Kahawa cha mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro, Moses Oguda amewaambia waandishi wa habari kuwa baadhi ya majalada ya kesi hiyo yamerejeshwa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kwa ajili ya utekelezaji.

Baadhi ya viongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Vyama vya Ushirika katika Kanda ya Kaskazini wanatuhumiwa kuuza nyumba za ushirika kisha kununua mtambo feki wa kukoboa Kahawa ambao haujafanya kazi tangu ununuliwe miaka minne sasa.

Pia TAKUKURU imepokea taarifa za rushwa zipatazo 15 na kuzifanyia kazi, nyingi kati ya hizo zikiwa ni kutoka idara za Elimu, serikali za mitaa, polisi na Mahakama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents