Habari

TAKUKURU waeleza mbele ya mahakama walivyomkuta gesti Mhadhiri wa NIT akimuomba rushwa ya ngono mwanafunzi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imeeleza mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam, Namna ilivyomkuta gesti Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (68) akiomba rushwa ya ngono.


Maelezo hayo yamesomwa leo Jumatano Oktoba 9, 2019 mahakamani hapo na wakili wa TAKUKURU,  Faraja Salamba wakati akimsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.

Wakili ameeleza kuwa, Salamba kwa kipindi hicho, Mhadhiri huyo alikuwa mwajiriwa wa NIT akifundisha wanafunzi wa muhula wa kwanza wa  2015/2016 somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji.

Mzee Mahimbo (68) anakabiliwa na kesi hiyo ya  kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa chuo hicho, Victoria Faustine.

Imeelezwa kuwa mnamo Januari 5 na 11, 2017 mshtakiwa alitumia madaraka yake vibaya kwa kuomba rushwa ya ngono na alimpigia simu Victoria na kumsisitiza wakutane katika baa ya Shani iliyopo maeneno ya Sinza Jijini Dar Es Salaam.

Salamba, Amesema Mhadhiri huyo alipokutana na mwanafunzi huyo kwenye Bar hiyo,  Alikuwa na mtihani na majibu ya marudio ya mtihani wa  Victoria wa somo alilokuwa akimfundisha na majibu, alimpa aufanye tena na alipomaliza akasahihisha na kumpa alama 67 na kumuomba rushwa ya ngono wakiwa Gesti.

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents