Habari

TAKUKURU wagundua njia mpya ya kutoa na kupokea rushwa, ni hii

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa imesema tatizo la rushwa bado ni kubwa nchini kutokana wanaojihusisha na vitendo hivyo kubuni mbinu mpya za kisasa za kufanikisha mipango hiyo.

takukuruccm_1
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, Valentino Mlowola.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, Valentino Mlowola, Jumanne hii wakati wa kongamano la wanafunzi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maadili na Haki za Binadamu.

“Sheria ya rushwa na mapambano yamekuwa yanaendelea yanabadilika kadri ya muda unavyokwenda. Leo hivi sasa tulikuwa na miaka hivi ya 70 kulikuwa na kikosi cha kupambana na rushwa tulikuwa tunaandaa hii mitego mitego, tunaenda kukaa mahali kuangalia watu wanaopokea rushwa tunawakamata. Lakini angalia changamoto za sasa hela inakwenda kwa tigo pesa lazima tubadilishe mbinu, social problem yoyote haiwezi kuwa kirahisi namna hiyo,” amesema Mlowola.

Hivi karibuni Rais Dkt John Magufuli akiwa ikulu na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa vyombo mbalimbali nchini alisema kuwa rushwa ni kansa ya maendeleo ya nchi na kumuomba kila mwananchi kuikwepa.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents