Habari

TAKUKURU yafanikiwa kurejesha fedha jumla ya Tsh bilioni 4 kutoka kwa watuhumiwa

Akizungumza na vyombo vya habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, alisema uchunguzi huo umefanywa kufuatia agizo lililotolewa na serikali kupitia kwa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kwa mamlaka hiyo baada ya uchunguzi mwingine kufanywa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) na kubaini mapungufu katika vyama hivyo.

“Mtakumbuka kwamba, takriban mwezi mmoja na nusu uliopita, Waziri wa Kilimo alinikabidhi muhtasari wa uchambuzi uliofanywa na Shirika la Usimamizi na Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika, Takukuru mpaka sasa tumefanikiwa kuchunguza Sh. bilioni 51, na wakati uchunguzi wa Sh. bilioni 72 unaendelea,” alisema Jenerali Mbungo

Alisema kuwa vyama vilivyofanyiwa ukaguzi ni 4,413 ikiwamo Vyama Vikuu 38, Amcos 2,710, Saccos 1,448 na vyama vingine 217 na kugundua fedha ambayo ilikuwa na viashiria vya ubadhirifu na rushwa kiasi cha Sh. bilioni 124, na kwamba mpaka sasa taasisi hiyo imefanikiwa kukagua miradi 51 na kufanikiwa kuokoa kiasi cha Sh. bilioni 4 zilizokuwa na viashiria vya rushwa

Katika ukaguzi uliofanywa na Coasco, hadi kufikia Juni 30, mwaka jana kabla ya ripoti hiyo kukabidhiwa kwa Takukuru, ulibaini kuwapo kwa vyama vya ushirika 11,410 vilivyosajiliwa na kati ya hivyo vyama hai ni 6,463 wakati vyama sinzia ni 2,844, huku vyama 2,103 vikiwa havijulikani vilipo

Mikoa iliyokaguliwa na kiasi cha fedha kilichookolewa ni Ruvuma Sh. 9,968,000, Kilimanjaro Sh. 38,075,967, Manyara Sh. 9,856,800, Katavi Sh. 49,000,000, Pwani Sh. 291,400,000, Mbeya Sh. 50,701,900 , Iringa Sh. 133,801,317, Simiyu Sh. 57,178,000, Arusha Sh. 1,256,000, Lindi Sh. 1,042,362,754 na Njombe Sh. 1,021,472,480

Mikoa mingine ni Mtwara Sh. 681,276,646, Songwe Sh. 354,374,673, Tabora Sh. 69,492,274, Tanga Sh. 10,842,480, Temeke Sh. 2,120,000 na Mara Sh. 242,982,800

Source: Nipashe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents