Habari

TAKUKURU yamtaja mmiliki vichwa vya treni vyenye utata

Mnamo mwezi Julai katika Bandari ya Dar es salaam vilikamatwa vichwa vya treni ambapo Rais Dkt Magufuli aliagiza vyombo vya uchunguzi nani hasa ni mmiliki wake baada ya umiliki wake kuwa na utata baada ya wizara ya Ujenzi wa Uchukuzi na Mawasiliano kutokuwa na taarifa za ununuzi wa vichwa hivyo.


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola

Akizungumza na Azam Tv, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola amesema kuwa mchakato wa kununua vichwa hivyo ulianza mwaka 2014/2015.

“Tumebaini kwamba mchakato wa kununua vichwa hivyo ushaanza mwaka 2014/2015 mchakato umeanza lakini haukufika mwisho na hakukuwa na mkataba uliosaini kwaajili ya vichwa hivyo kufika nchini au kununuliwa nchini, shirika linalohusika na usafirishaji wa reli ulianza mchakato wa kuanza kununua hivyo vichwa lakini hapakuwa na mkataba wa mauziano wale walileta kwa matumaini kwamba tu vitanunuliwa,” alisema Mlowola.

“Mmiliki yupo na mmiliki ni yule aliyetengeneza na kuvileta hapa nchini anajulikana ni kampuni ya electro Modern ya nchini Marekani ndo ilivileta hapa nchini, lakini hakuna mkataba wa maridhiano kati ya shirika la reli Tanzania(TRL) na wao japo mazungumzo yalikuwepo huko nyuma,” aliongeza Mlowola.

Mlowola alieleza hatua ambazo wamechukua baada ya kubaini hayo “Katika uchunguzi wa aina hii kuna vitu vingi vinatokea inawekekana kuna taratibu za Kiutawala zilikiukwa au makosa ya jinai yalitendwa sasa hatua inaanza baada ya kuona nini kilifanyika so far tulipofikia tunaliangalia watuhumiwa wote,wahusika wote wameshahojiwa vielelezo vyote vilipatikana na kama kuna hatua nyingine basi kwa utararibu wetu tunapeleka jalada letu kwa Mwanansheria wa Serikali, muendesha mashtaka wa serikali na yeye akibaini kwamba kuna makosa ya jinai ambayo yametendwa tunakwenda Mahakamani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents