Habari

TAKUKURU yawaburuza wawili Mahakamani, James Rugemalira ndani

By  | Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema imewafikisha watuhumiwa wawili ambaye ni bwana Harbinder Singh Sethi na James Rugemalira kwa kosa la uhujumu uchumi.

Hayo yamezungumzwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Valentino Mlowola wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Leo tunawapa taarifa kwamba tunawafikisha Mahakamani watuhumiwa wawili bwana Harbinder Singh Sethi na James Rugemalila na hawa tuna wafikisha Mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi na makosa mengine yanayo hayo kwa muda mrefu sana nimekua naulizwa kesi za ESCROW na IPTL imeishia wapi, kama tulivyosema mwanzo kwa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na kuzuia rushwa na makosa ya ufisadi,” alisema Mlowola.

“Kwahiyo katika muendelezo wa majukumu yetu tulichunguza jukumu hili kwa muda mrefu na sisi umefika wakati muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa wakuu hawa wa mashauri ya kuhujumu uchumi wa nchi yetu Mahakamani, kwahiyo kwa wale mtakao waona Mahakamani wameshapelekwa Mahakamani.”

Aidha Mlowola ametoa wito kwa wananchi “Nataka nitoe wito kwa Watanzania kwamba serikali ina nia nzuri na dhati ya vitendo vya kuhujumu uchumi wa nchi yetu ili wananchi wapate maisha bora zaidi na jukumu hili TAKUKURU tutaendelea kulitekeleza kwa nguvu zetu zote kwa weledi wetu wote na kwa umakini wa hali ya juu na kuhakikisha kwamba vitendo vyote vya kuhujumu uchumi vinadhibitiwa ili wananchi wapate maisha bora.”

Na Emmy Mwaipopo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments