Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Takwimu na nafasi ya Man United kundi H michuano ya UEFA kabla ya mchezo wa leo,Mourinho asema “Mchezo wa leo sio kipaumbele kwangu”

Takwimu na nafasi ya Man United kundi H michuano ya UEFA kabla ya mchezo wa leo,Mourinho asema "Mchezo wa leo sio kipaumbele kwangu"

Leo usiku kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka ambako Manchester United wataifuata Juventus katika jiji la Torino kwenda kukamilisha mchezo wao wa pili ikiwa mchezo wa kwanza United alipoteza nyumbani kwao katika dimba la Old Trafford kwa kupigwa goli 1-0.

Ikumbukwe kwamba, Juventus mpaka sasa haijaruhusu bao lolote kwenye nyavu zao na wana alama 9. Wana uhakika wa kufuzu. Shida ipo hapa kwenye nafasi ya pili. United vs Valencia.
United wasipokuwa makini huenda wakakwama endapo mchezo wao leo huko Turin watakosa alama yoyote.

Hizi ni Takwimu za United vs Juventus:-

DateMatchResultScoreCompetition
20 Oct 1976Manchester United v JuventusW1-0UEFA Cup
03 Nov 1976Juventus v Manchester UnitedL3-0UEFA Cup
11 Apr 1984Manchester United v JuventusD1-1UEFA European Cup Winners Cup
25 Apr 1984Juventus v Manchester UnitedL2-1UEFA European Cup Winners Cup
11 Sep 1996Juventus v Manchester UnitedL1-0UEFA Champions League
20 Nov 1996Manchester United v JuventusL0-1UEFA Champions League
01 Oct 1997Manchester United v JuventusW3-2UEFA Champions League
10 Dec 1997Juventus v Manchester UnitedL1-0UEFA Champions League
07 Apr 1999Manchester United v JuventusD1-1UEFA Champions League
21 Apr 1999Juventus v Manchester UnitedW2-3UEFA Champions League
19 Feb 2003Manchester United v JuventusW2-1UEFA Champions League
25 Feb 2003Juventus v Manchester UnitedW0-3UEFA Champions League
23 Oct 2018Manchester United v JuventusL0-1UEFA Champions League
07 Nov 2018Juventus v Manchester UnitedUEFA Champions League
Kwa takwimu hizo Manchester United wamefanikiwa kuifunga Juventus michezo 5 na Juventus wakishinda michezo 6 huku sare zikiwa 2:-


Mourinho amesema hatahangaika na mchezo wa leo kwan bado ana michezo miwili ukiweml wa Young boys Old Trafford. Kama Valencia wataifunga Young boys, watafikisha alama 5. Kama United akifanikiwa angalau kupata sare Turin watalingana alama 5. United itahitaji ushindi wa lazima dhidi ya Young boys pale Old Trafford, huku wakiomba Juventus iwafunge Valencia kisha mchezo wao wa mwisho utoke na matokeo ya aina yeyote ile.


Takwimu za United Vs Valencia.

02 Oct 2018: UCL [Man Utd 0 – 0 Valencia] 07 Dec 2010: UCL [Man Utd 1 – 1 Valencia ] 29 Sep 2010: UCL [Valencia 0 – 1 Man Utd] 20 Feb 2001: UCL [Man Utd 1 – 1 Valencia] 14 Feb 2001: UCL [Valencia 0 – 0 Man Utd ] 21 Mar 2000: UCL [Valencia 0 – 0 Man Utd ] 08 Dec 1999: UCL [Man Utd 3 – 0 Valencia ] 29 Sep 1982: UEFA CUP [Valencia 2 – 1 Man Utd ] 15 Sep 1982: UEFA CUP [Man Utd 0 – 0 Valencia ]

Ni miaka 36 tokea Valencia waifunge Man United, Huu utakuwa wakati muafaka wa United kulipa kisasi kwa wahispania baada ya Sevilla kuwatoa United hatua ya 16 bora msimu uliopita.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW