Burudani

Tamasha la Nyama Choma kufanyika Dar Jumamosi hii, March 8

Kwa mara ya kwanza kabisa mwaka huu 2014, lile tamasha kubwa la Nyama Choma linalofahamika kama The Nyama Choma Festival (TNCF) limepangwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2014.

Ticket deals2-03

Nani alifikiria kuwa Nyamachoma ingeweza kuwaleta maelfu ya watu pamoja? Toka lilipoanzishwa, tamasha la nyama choma ambalo limesajiriwa kisheria limekuwa ni sehemu ya kipekee ya kuweza kufurahia aina mbalimbali za nyama choma na pia ni eneo linalowakuwakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali wanaofika kufaidi nyama zinazochomwa na wataalamu wa kuchoma nyama kutoka katika kona mbalimbali za jiji la Dar salaam kwa kiingilio cha shilingi 10,000 tu.

TNCF 5

Ukiachana na aina mbalimbali ya nyama zinazokuwepo katika tamasha hili, hii pia ni sehemu mojawapo ya kufurahi na marafiki ikiwa ni pamoja na “mtoko” kwa familia kwani huduma zinazotolewa zimezingatia umri wa watu wote yaani kuanzia watoto hadi watu wazima. Kuna eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya michezo ya watoto, vinywaji vya ain azote na burudani nzuri ya muziki. Si hivyo tu wapo watu wengine wanaotoa huduma za kahawa, ice cream, michoro ya usoni, vyakula vya kawaida na michezo ya nje ya watuwazima kama pool n.k

Tupo katika dunia ambayo inatulazimu kuwa katika mtandao mkubwa na watu wenye weledi tofauti, The Nyama Choma Festival inakuwezesha kuingia katika mtandao huu kwa urahisi zaidi. Kwani kwa siku hii moja tu watu wote wanaweka vyeo na nafasi zao kitaaluma pembeni na kuchanganyika na watu wote huku wakifurahi kwa pamoja. Katika hali hii watu wanabadilishana uzoefu na kupeana mawasiliano kwa ajili ya siku za usoni.

TNCF 2

Nyamachoma inawawezesha watu hawa wenye weledi tofauti ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa maofisini na wafanyabiashara kuja kwa pamoja kuzungumza changamoto zao kikazi na kushirikiana kwa ukaribu hapo baadae katika majukumu mengine ya kimaendeleo kupitia taaluma na weledi wao.

Mwaka huu Nyama choma imeamua kuongeza wigo wake zaidi katika sehemu mbalimbali nchini. Ukiachana na Dar es salaam TNCF ilishafanyika Moshi, Arusha na Mwanza na kwa mwaka 2014 itaendelea katika mikoa ifuatayo (Tarehe zinaweza kubadilika)

• Dar es Salaam 08 Machi
• Arusha 26 Aprili
• Mwanza 4 Mei
• Dar es Salaam 7 Juni
• Dodoma 3 Agouti
• Morogoro 24 Agosti
• Dar es Salaam 6 Septemba
• Mwanza 26 Oktoba
• Dar es Salaam 6 Desemba
• Moshi 26 Desemba

Toka kuanzishwa kwake TNCF ilipangwa kuwa Tamasha kubwa na maarufu linalofanyika mara nne kwa mwaka likiwakilisha mila ya kitanzania kwa utaalamu wa kuchoma nyama katika miji ambayo inapenda sana nyama choma. Nyama choma ni chakula maarufu kwa wakazi wa Afrika Mashariki, na hasa kukiwa na matukio maalumu na hii ndio maana maelfu ya watu wanafika katika tamasha hili. Kwa kiingilio kimoja tu kisicha na matabaka kwa wote, unapata nafasi ya kuchagua kununua nyama kutoka katiko majiko tele yaliyojazana katika viwanja hivi.

Na kwa ukarimu wa kitanzania, kila atakayeingia atapewa mshikaki mkubwa na ulionona getini pamoja na kinywaji kisicho na kilevi getini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents