Burudani

Tamko la Mr Nice kwa mashabiki wake

Mr_Nice_face_2

Mwanamuziki ambaye ameweza kuitangaza Tanzania nje ya nchi kupitia muziki wa Bongo Fleva, hasa kwa kubuni staili mpya ya uimbaji na uchezaji TAKEU ikiwa na maana Tanzania, Kenya, Uganda ambayo ilikuja kuwa gumzo Afrika mshariki na kati, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ ametoa tamko kwa mashabiki wake juu ya kurudi tena kwenye Game baada ya kimya cha muda mrefu.
Mr Nice amechonga na BONGO5, na kusema kwamba kwa sasa amejipanga baada ya kupokea ujumbe mwingi kwa mashabiki wake wa Afrika nzima, baada ya kuona kimya chake kwa takribani miaka saba, tangu alipoachia kitu chake cha mwisho cha bwana Shamba.

Mr_Nice_ramar

Aidha amesema kwamba kwakuwa yeye ndiyo aliyeianzisha staili hiyo, na htmaye wasanii wengine kushindwa kuiendeleza hivyo, hata mashabiki wa staili hiyo pia wakamuomba aje aindeleze mwenyewe kwani radha ya staili hiyo ya TAKEU imekuwa ikipotea siku hadi siku.

Mr Nice amesema kwa sasa meamua kurudi na staili ile ile ila kwa sasa ameiboresha zaidi na kuita TAKEU Reloaded, akiwa na maana kurudi kwa staili hiyo lakini ikiwa ya kisasa kulingana na muziki wa Bongofleva unavyokwenda, pia ameiboresha ili kufanya ipendwe zaidi ya mwanzo

Mr_Nice_Dunga

Amesema katika kukamilisha mahitaji ya mashabiki wake ambao wamekuwa wakimwitaji kwa siku zote, ndipo alipoamua kuungana na Ramar pamoja na Dunga, katika kuleta mabadiliko hayo, huku akiwa tayari ameshakamilisha nyimbo sita kwaajili ya albamu yake ambayo itakuwa ni bora zaidi.

Amesema katika albamu yake hiyo itakuwa na nyimbo kali sita ambazo zote zipo katika mtindo huo mpya wa TAKEU reloaded, ambapo Ijumaaa hii anatarajia kuachia nyimbo ya Tabia ambayo itakuwa gumzo, na pia yupo katika mikakati ya mwisho ya kuandaa video ya wimbo huo.

Mr Nice anakumbukwa sana kwa staili hiyo kwa nyimbo zake kali kama Fagilia, King’asti, Friday Night, Bwana Shamba na nyingine nyingi ambayo pindo zilipokuwa zikipigwa hakuna ambayo hakuonyesha ushirikiano katika kuimba, au kucheza na hata kutingisha kiungo kwa yule aliyeshindwa vyote.

Mr_Nice_face

Huyo ndiyo Mr Nice na Ujumbe wake kwa mashabiki, na hii ni moja ya nyimbo ambayo ilikuwa ikisumbua sana kwa kipindi hicho… Mwisho anawaomba Watanzania kumuunga mkono ili aweze kuufikisha muziki wetu mbali kama ilivyokuwa kwa mwanzo.

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=Zd83HZFlelU[/youtube]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents