Burudani

Tamu wa kundi la BongoLos aelezea ukweli huu kuhusu maisha yake

By  | 

Member wa kundi jipya la muziki ‘BongoLos’ amefunguka na kuelezea maisha yake ya kimahusiano na ya utafutaji yalivyokuwa kabla ya kujiunga na kundi hilo.

Tamu

Tamu amekiambia kipindi cha Kwetu Flavor kwamba,kwa sasa ana mtoto wa mwaka mmoja lakini baba mtoto wake hawapo tena pamoja kutokana na kushindwa kutofautiana kipindi alipokuwa mjamzito.

“Nilishawahi kuishi na mwanaume tukakaa kwa mwaka mmojana miezi nane, nikabeba mimba lakini baadaye tukawa hatuelewani, nikaondoka nikiwa na mimba, na mtoto wangu yupo sasa ana mwaka mmoja sasa hivi,” amesema Tamu.

Katika hatua nyingine msanii huyo amesema alikuwa anafanya kazi ya kuagizwa baadhi ya vitu kama nguo na simu, kazi ambayo ilimuwezesha yeye kuishi.

“Nilishawahi kufanya mishe mishe town zile unachukua mzigo duka hili unapeleka kule, unachukua simu unampelekea mtu, kuna matajiri hawataki kutoka kwenda dukani kuangaika kwa hiyo mimi nawapelekea mzigo,” amesema kuongeza.

“Mimi nilikuwa ninatumwa, issue kwamba kuna mzigo huu hapa wa nguo peleka duka fulani, kuna mzigo wa simu peleka duka fulani unaweza ukapata pesa ya nauli na ukapata pesa ya chakula,” ameleza Tamu.

By Peter Akaro

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments