Habari

TANESCO yaendelea kuilipa Richmond mamiloni

Licha ya Kamati ya Bunge kupendekeza kufutwa kwa mkataba wa Richmond na kutaka malipo ya Sh. milioni 152 yanayotolewa kwa Dowans kila siku yasitishwe hadi jana Shirika la Umeme(TANESCO) liliendelea kuilipa kampuni hiyo.

Na Restuta James

 

 

 
Licha ya Kamati ya Bunge kupendekeza kufutwa kwa mkataba wa Richmond na kutaka malipo ya Sh. milioni 152 yanayotolewa kwa Dowans kila siku yasitishwe hadi jana Shirika la Umeme(TANESCO) liliendelea kuilipa kampuni hiyo.

 

 

 

Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bw. Daniel Mshana aliliambia gazeti hili jana katika mahojiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kuwa shirika linasubiri maelekezo kutoka serikalini.

 

 

 

Alitoa ufafanuzi huo alipoulizwa iwapo TANESCO imejipanga kusitisha malipo hayo na pia aliulizwa kiasi cha fedha kilicholipwa kwa kampuni hiyo tangu kuanza kwa mkataba huo uliosainiwa mwaka jana.

 

 

 

“Bunge lilijadili suala hili na kupendekeza hivyo lakini hatujasitisha malipo maana serikali haijaanza kutekeleza pendekezo hilo. Nadhani bado ipo katika mchakato wa kuyapitia na kufanya taratibu kwa mujibu wa maelekezo,“ alisema.

 

 

 

Alipoulizwa lini mkataba utasimamishwa alisema ni jukumu la Wizara ya Nishati na Madini kuamua wakati wa kuchukua hatua hiyo.

 

 

 

Waziri wa wizara hiyo, Bw. William Ngeleja, alipoulizwa juu ya kusimamisha mkataba huo alisema hatma ya jambo hilo ipo mikononi mwa kamati ya sekta mbalimbali iliyoundwa na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda kupitia na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo hayo.

 

 

 

“Tupeni muda kidogo wakati kamati ile inachambua mapendekezo maana wao watatoa mwelekeo mzuri katika utekelezaji ripoti ya Bunge,“ alisema.

 

 

 

Alifafanua kuwa hata kama Dowans wataendelea kulipwa hatua za kisheria zitachukuliwa kurudisha fedha iwapo italazimika kufanya hivyo.

 

 

 

Wiki iliyopita, Bunge lilipitisha mapendekezo 23 yaliyotolewa na kamati yake likiwemo suala la kusitisha malipo ya Sh. milioni 152 kwa kampuni ya Dowans mapema iwezekanavyo.

 

 

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents