Burudani ya Michezo Live

Tanga walivyofurahia msimu wa dhahabu

 

Fiesta_Tanga_Prof_J_face

MAELFU ya wakazi wa Jiji la Tanga, Jumapilii iliyopita walihitimisha ziara ya Serengeti Fiesta ya 10 upande wa mikoani, baada ya kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo lililofanyika katika uwanja wa Mkwakwani.


Burudani toka kwa wasanii mbalimbali iliyoporomoshwa kwa zaidi ya Saa 9, ilikuwa tosha kuwafanya wakazi hao wajisikie ‘majotroo’ na hivyo kuamsha shangwe zisizo na kifani.

Tamasha hilo ndilo la mwisho mikoani tangu lizinduliwe takribani mwezi mmoja uliopita katika Jiji la Mwanza, huku likitarajiwa kuhitimishwa rasmi wikiendi hii Jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders Club.

Fissta_Tanga_Tip_Top

Wasanii mbalimbali kutoka katika Jiji hilo la ‘waja leo, warudi leo’ ndio walikuwa wa kwanza kuwapagawisha wakazi wenzao tangu kuanza kwa tamasha hilo  Saa 10 za Jioni na baadaye kufuatiwa na wasanii wengine waliosafiri kwenda katika Jiji hilo kwa ajili ya kutoa burudani.

Wasanii toka kundi la Tipo-Top Connection,  Bell 9, Bob Junior, Mataruma, Ben Paul,Rechor,Ali Kiba na wengine wengi wa miondoko ya bongo fleva, walitoa  burudani tosha kwa mashabiki hao kutokana na nyimbo zao mbalimbali zinazotamba katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Fiesta_Tanga_Linex

Mwanamuziki Linex mkali wa mama Halima, akigonga vitu vyake.

Fiester_Tanga_Bob_Junior

Bab Junior Mr Chocorate Flevour akivunja katika msimu wa dhahamu T.A …..Tanga haina Majotroooo

Fiesta_Tanga_watu

Kam watu nyomi jijini Tanga ilikuwa hivi , kasheshe jumamosi hii ndani ya Leaders Club kwenye jiji la maraha, jiji lenye sifa zake, jiji lilozaliwa kwaajili ya burudani Dsm, Dar, Bongo au ukipenda unaweza kuliita Dar es salaam sijui itakuwaje……. Msimu wa dhahabu……….Haina majotrooooooooo.

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW