Burudani

Tangazo hili la mipira ya kiume ‘Condoms’ lazua gumzo nchini Kenya, serikali yatoa agizo (+video)

Tangazo la mipira ya kiume “Condoms’ lijulikanalo kwa kama Socks Condom limezua gumzo nchini Kenya baada ya wazazi kulalamika kuwa linasababisha watoto wao kuwaomba wanunuliwe soksi zinazofanana na mipira hiyo.

Dkt. Ezekiel Mutua kushoto kwenye picha

Tangazo hilo linaonesha wanaume kadhaa wakivalishwa soksi na wenza wao miguuni, ambapo soksi hizo ndio mipira ya kiume tayari limepigwa marufuku na serikali kuchezwa kabla ya saa nne usiku kwenye runinga.

Akizungumza na vyombo vya habari nchini Kenya Jana Agosti 31, 2018, Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza La kuthibiti Filamu nchini Kenya (KFCB), Dkt. Ezekiel Mutua amesema kuwa hata yeye nyumbani amekuwa akisumbuliwa na watoto wake awanunulie soksi kama hizo zinazoonekana kwenye tangazo hilo.

Kwa upande mwingine, Mutua ameyataka Makampuni ambayo yanajihusisha na matangazo kuwasilisha kazi zao kwenye Bodi ya Filamu nchini humo kwani hata tangazo hilo limekiuka vifungu vya sheria.

Baada ya mkutano huo, Dkt Mutua amesema kuwa tangazo hilo litapeperushwa tu kuanzia saa nne usiku wakati ambao kwa asilimia kubwa huwa wamelala.

Tutafanya kazi kwa ushirikiano na maprodusa, watengenezaji wa adverts na washikadau wote ili kuwalinda watoto wetu kutokana na contents ambazo zinawapotosha,” amesema Dkt Mutua.

Katika tangazo hilo, panaonekana Wanaume ambao wanavalia soksi kwa njia tofauti kisha mwisho wa tangazo panatolewa mfano wa njisi ya kuvalia soksi (kondomu).

Wakenya walikuwa wakilalamikia tangazo hilo ambalo pia linachezwa mchana peupe na watoto walikuwa wameanza kuiga maneno ambayo yanatumiwa katika tangazo hilo.

By Moses Njonge.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents