Burudani

Tangu video kuvuja: Bill Nass na Nandy wamekutana polisi tu

Msanii Bill Nass amesema tangu ilipovuja video yake ya faragha akiwa na Nandy, wamekutana mara moja tu.

Hata hivyo hilo halimaanishi kuna kitu hakipo sawa kati yao, hapana!, wao bado ni marafiki na kilichotokea ni sehemu ya kujifunza.

“Tangu niliporudi nimeonana na Nandy mara moja tu, siku tulipoenda polisi kutoa maelezo nini kimetokea, nilizungumza nae tu kutaka kufahamu kuhusiana na kesi iliyopo polisi,” amesema.

“Nandy ni rafiki yangu, yaliyopita ni sehemu ya kujifunza maisha na kuhakikisha huko mbele jambo hili halijitokezi tena,” Bill Nass ameiambia XXL, Clouds FM.

Soma Pia: Wakubwa Tu +18: Video ya utupu ya Nandy na Bill Nass yavuja mtandaoni

Bill Nass ameongeza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ni nani aliyesambaza hiyo video.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents