Burudani

Tanzania hakuna management kuna madalali – AT

Mwimbaji wa muziki wa mduara AT amesema wakati yupo chini ya management alikuwa haoni faida ya muziki wake.

AT

Akizungumza na Story Tatu ndani ya kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, AT amesema Tanzania hakuna mameneja wa muziki bali kuna madalali.

“Tanzania hakuna management kuna madalali tu,” alisema. “Wakati nasimamiwa nilikuwa sioni faida ya muziki ninaofanya lakini baada ya kuanza kujisimamia mimi mwenyewe kama mimi, nilipata kuelewa kwanza muziki ukoje na una ugumu gani, na kipato chake ni kipi,” alisisitiza.

“Meneja maana yake ni mfanyakazi wa msanii, lakini Tanzania meneja ni bosi analala anategemea msanii apate show yeye ndo ale. Yeye hawezi kutafuta show, meneja hawezi akamkodia msanii nyumba, gari, akamtengeneza msanii sera za kule anakokwenda. Anachosubiri ni show, akishakuona unaanza kulegalega uwezo umepungua anakuacha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents