Burudani

Tanzania hatuna Super Star kwenye muziki – One the Incredible

Msanii wa Bongo Fleva, One the Incredible amedai Tanzania kwa sasa hatuna super star katika tasnia ya muziki kwa kuwa hakuna msanii aliyewahi kuingiza wimbo Billboard top 100.

Rapper huyo amekiambia kituo cha radio cha Time FM, pengine ma-super star wapo katika tasnia nyingine lakini sio muziki.

“Mimi ili wewe nikukubali kama super star, kama haujawahi kuingiza wimbo Billboard wewe sio super star ni kwamba unakubalika kwenye maeneo fulani fulani ya Africa, Europe na Marekani, lakini tunajua industry inavyofanya kazi, itakutangaza ujione ni mkubwa kwenye eneo lako kwa sababu wimbo wako inapigwa kila sehemu unaonekana kwenye mabango, unapewa matangazo, unapata hela lakini ule ni uongo,” amesema One.

“Ili uitwee super star inabidi kumvuka marehemu mtoto wa Dandu, ndio msanii pekee Tanzania toka historia ya muziki imewahi kuingiza wimbo wake kwenye Billboard top 100. Tuna wasanii wakubwa wana-coverage, wana-platform na ninawaheshimu kwa sababu wameweza kufika hatua hiyo lakini sio super star,” amesistiza One the Incerible.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents