Habari

Tanzania kukumbwa na ukame

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), imesema mtawanyiko hafifu wa mvua na vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha msimu wa mvua wa Oktoba hadi Desemba mwaka huu huku wakiwaasa wafugaji kuuza mifugo yao mapema ikiwa bado ina hali nzuri.

Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi leo Jumatatu kwenye Mkutano na waandishi wa Habari, kuwa mikoa itakayoathirika ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Wafugaji wanashauriwa kuvuna mifugo yao ikiwa katika hali nzuri kiafya na pia kuvuna maji na wahifadhi malisho ili kukidhi mahitaji katika kipindi cha upungufu,” amesema Dkt Kijazi.

Hata hivyo, Dk Kijazi amezitaka mamlaka husika kama vile wadau wa afya, menejmenti za maafa, mamlaka za miji na wadau wengine kuchukua hatua stahiki katika kupunguza athari mbaya zinazoweza kutokea katika msimu wa mvua za vuli 2017.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents