Moto Hauzimwi

Tanzania Music Awards yanukia

Tuzo za Tanzania Music Awards kwa mwaka huu 2006 na ambazo hudhaminiwa na Tanzania Breweries kupitia bia yake ya Kilimanjaro zitatolewa May mwaka huu.


Tuzo za Tanzania Music Awards kwa mwaka huu 2006 na ambazo hudhaminiwa na Tanzania Breweries kupitia bia yake ya Kilimanjaro zitatolewa May mwaka huu.

Hayo yalisemwa kwenye uzinduzi wa tuzo hizo uliofanyika juzi usiku ndani ya ukumbi wa NSSF Water Front na kuhudhuriwa na wasanii pamoja na wadau wa muziki hapa nchini.

Akiongea na waliohudhuria uzinduzi huo,Manager wa Bia ya Kilimanjaro Oscar Makoye alisema tuzo hizo kabla ya yote zitatanguliwa na mchakato wa kuwapata wasanii watakaowania tuzo hizo.

Akiendelea alisema zoezi zima la upigaji wa kura kwa ajili ya kuwapendekeza wasanii wataongia kwenye tuzo hizo litakwenda kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi kwa kutumia mtandao wa Celtel na kazi hiyo inatarajiwa kuanza April 8.

Katika uzinduzi huo uliofana kulikua na burudani mbalimbali ambapo wasanii kadhaa walitoa show wakiwemo TOK kutoka Jamaica,TMK Majita na wengineo.

Kwa kawaida baada ya tuzo, wasanii waliojinyakulia tuzo hizo hupata nafasi ya kutembelea mikoa karibu yote ya Tanzania kuwaburudisha watanzania.

  • SOURCE: Darhotwire

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW