Tia Kitu. Pata Vituuz!

Tanzania Music Power Ent. kutoa tuzo ya ‘Best Couple 2013’ kwenye Valentine’s Day

valentines couples 2 copy (618x800)

Kampuni ya Tanzania Music Power Entertainment ya jijini Dar es salaam ikishirikiana na Hotel Demag imeandaa tuzo kwa wapendanao kwa mwaka 2013.

Hizo ni tuzo za mara ya kwanza kufanyika nchini ambapo kwa mwaka huu zitawatuza wapendanao wawili walio mfano wa kuigwa katika jamii katika kudumu kwao katika mapenzi kwa kuvumiliana. Pia wapendanao hao wawe wameweza kwa pamoja kurudisha kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa ajira au mchango mbalimbali kwa wahitaji.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Music Power Entertainment, Phabian Duwe akifafanua jambo wakati wa kutangaza tuzo za wapendanao zitakazofanyika Februari 14 kwenye Hoteli ya Demag iliyopo  Mwananyamala jijini Dar es  Salaam. Katikati ni Meneja wa TMPE, Evelyn Munisi na Ludovick Mugasha.

Kutokana na hilo kampuni ya TMPE imeona umuhimu wa kuwazawadia tuzo wapenzi wa namna hiyo kwa kutambua mchango wao katika jamii na kudumu katika mahusiano kwa muda mrefu bila mfarakano ulionekana wazi hadi katika jamii.
Kampuni hiyo itatoa tuzo hiyo ya The Best Couple 2013 kwa mtu yeyote katika jamii bila kujali itikadi yake ambapo anaweza kuwa mbunge,msanii wa muziki ama filamu, waziri ama mtu yeyote maarufu nchini.

“Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana kupitia tafiti zetu katika vyombo vya habari mbalimbali,magazeti,runinga,radio,mitandao mbalimbali ya kijamii n.k ambaye kimsingi mshindi wa tuzo hiyo sharti anatakiwa awe hajaripotiwa vibaya au kuwa na skendo mbalimbali zinazomchafua,” imesema kampuni hiyo kwenye maelezo yake.

Mwanamuzi, Rogers Lucas atakayetoa burudani katika utoaji wa tuzo hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Phabian Duwe na Meneja wa TMPE, Evelyn Munisi.
Mwanamuzi, Rogers Lucas atakayetoa burudani katika utoaji wa tuzo hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Phabian Duwe na Meneja wa TMPE, Evelyn Munisi.

“Tukio hilo litafanyika siku ya wapendanao, February 14, 2013 katika hotel ya Demag iliyopo Mwananyamala Komakoma, Dar es salaam ambapo pia kutakuwa na kiingilio, wapendanao wawili( valentine couples) sh.70,000/= ambayo itajumuishwa na buffet, vinywaji,kuogelea na cocktail na single sh,50,000/= itajumuishwa huduma hizo za kwanza ambapo pia kutakuwa na burudani ya muziki wa live,mwanamuziki Rodgers Lucas aliyekuwa mshindi wa pili katika shindano la BSS 2011 atakayetoa burudani ya uhakika kupitia gitaa lake live na vilevile kutakuwa na surprise kibao za burudani na zawadi.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW