Moto Hauzimwi

Tanzania na Uganda tutaendelea kuimarisha ushirikiano wetu – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na kidiplomasia baina yake na Uganda.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania Bw. Richard Tumusiime Kaonero, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 12, 2017
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Bw. Richard Kaonero jijini Dar es Salaam.

“Tunaimani kubwa na ushirikiano wetu na Serikali ya Uganda. Tutaendelea kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo tunayoitekeleza kwa pamoja ukiwemo ujenzi wa bomba la gesi,”amesema Waziri Mkuu.

Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uganda ili waje kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo.

Pia amewakaribisha raia wa Uganda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na mbuga za wanyama.

Kwa upande wake, Balozi Kaonero ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW