Habari

Tanzania nayo yajipanga kuzizima simu bandia

Tanzania inatarajia kuchukua hatua kama iliyochukuliwa nchini Kenya ya kuzichinjia baharini simu zote za bandia ambazo nyingi ni za kichina kwa kuzizima kabisa.

Taarifa hiyo imetolewa na kaimu meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano (TCRA) Semu Mwakyanjala ambaye amesema mamlaka hiyo itaanza kwa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na umuhimu wa kununua simu halali.

Ameliambia gazeti la Daily News Jumapili kuwa hatua hiyo itachukuliwa na nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Rwanda, Uganda na Burundi.

Kuna taarifa kuwa makampuni mengi ya simu nchini Tanzania yameupokea mpango huo kwa shingo upande kwa hofu kuwa yatapoteza wateja wengi.

Kwa upande wa tume ya mawasiliano ya Uganda (UCC) hatua hiyo ya kuzima simu bandia itafanyika mwishoni mwa mwezi November.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents