AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Tanzania tukikosa misaada tutaishi, tuna rasilimali na uongozi bora – Dkt. Bashiru

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa kwa sasa Serikali inayoongozwa na chama hicho haitakubali kupokea misaada yenye masharti magumu.

Dkt. Bashiru Ally

Bashiru amesema hayo jana mkoani Mwanza, kwenye ziara yake ya siku mbili ya kikazi.

Tunataka kujenga uchumi wa nchi wa yetu na kulinda uhuru wa Taifa letu. Ni kupitia siasa ya uchumi wa kujitegemea, na tumeanza kujitegemea kweli kweli. Wale ambao wanataka kutupa misaada kwa masharti magumu , hatupo tayari kupokea misaada kwa masharti. Sisi ni taifa huru, msiwasikilize wale wanasiasa ambao wamehamishia siasa zao kwenye ofisi za mabalozi, wanataka nchi yetu ikose misaada. Sisi hata tukikosa misaada tutaishi, tuna rasilimali nyingi, tuna watu, tuna uongozi bora. Hayo ndiyo ambayo yanaweza kutuhakikishia uhuru na maendeleo ya taifa letu.”amesema Dkt. Bashiru .

Kwenye ziara hiyo, Dkt. Bashiru atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mwanza.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW