Tanzania vs Tunisia, tuiombe Taifa Stars – Rais TFF Wallace Karia (+Video)

Rais wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati Cecafa na ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amewaomba Watanzania kuiombea timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars kuhakikisha hii leo usiku inachomoza na ushindi dhidi ya Tunisia kwenye mchezo wa ‘Group J’ mchezo wa kufuzu AFCON 2021 utakaopigwa uwanja wa Mkapa saa 4:00 usiku.

 

Karia ambaye pia ni Rais wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati Cecafa amezungumzia mashindano ya Cecafa ya U20 yatakayoanza kutimua vumbi tarehe 22 katika Mkoa wa Arusha na Karatu nchini Tanzania.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 2 Disemba na kushirikisha jumla ya timu tisa (9).

Wallace Karia amesema dhana yake ni kuhakikisha ausambaza mchezo wa mpira wa miguu katika sehemu mbalimbali.

”Matarajio yangu katika kipindi changu tutaziacha timu zikiwa juu katika Rank ya FIFA tofauti tunavyotazamwa sasa hivi ziko chini. Tulichukua U17 Boys, mwaka jana tukachukua U20 Girls na mwaka huu tumekwenda kuchukua U17 Girls kwa hiyo timu zetu zinafanya vizuri.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW