Tanzania Waweka Alama Silaha

TANZANIA imeanza kuweka alama katika silaha zote sambamba na nchi nyingine za Ukanda wa Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika.

TANZANIA imeanza kuweka alama katika silaha zote sambamba na nchi nyingine za Ukanda wa Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika.
Lengo la zoezi hilo ni kudhibiti uhalifu na kuzagaa kwa silaha pamoja na kuweka kumbukumbu nzuri za silaha zilizopo nchini.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna Robert Manumba, wakati akifungua warsha ya mafunzo ya uwekaji alama silaha iliyofanyika katika ukumbi wa Haidery Plaza, jijini Dar es Salaam.
Manumba alisema hapa nchini kuna mashine moja ya kuwekea alama hizo na kwamba uwekaji alama hizo ni utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya kimataifa kuhusu udhibiti wa silaha.
Katika Ukanda wa nchi za Maziwa na Pembe ya Afrika, utafanyika kwenye nchi 12 ambazo ni Tanzania, Uganda, Sudani, Kenya, Somalia, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Djibuti, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Somalia na kila nchi itakuwa na alama na namba yake ya utambuzi wa silaha.
“Uwekaji alama utasaidia na kumbukumbu nzuri zaidi ya silaha zilizopo nchini pamoja na kurahisisha ufuatiliaji wa vyanzo vya silaha,” alisema Manumba na kuongoza:

“Hadi sasa mashine tuliyopata kwa ajili ya kuweka alama ni moja tu na tutaanza kuitumia kuweka alama silaha zinazomilikiwa na Jeshi la Polisi na baadae Jeshi la Magereza na Mashirika ya Ulinzi ya watu binafsiā€.

Alifahamosha kuna wafadhili ambao wameonyesha nia ya kulipatia Jeshi la Polisi mashine nyingine zaidi ili kazi hiyo ikamilike haraka.

Aliongeza kuwa mashine zitakazokuja baadaye zinakabidhiwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuweka alama kwenye silaha zake.

Warsha hiyo ilihudhuriwa na washiriki kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Idara ya Usalama wa Taifa, Wanyama Pori, Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyama Pori (Tanapa).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents