Habari

Tanzania yaianza vibaya Olimpiki

Jana Tanzania imeyaanza vibaya mashindano ya Olimpiki baada ya bondia Selemani Kidunda kushindwa kutamba mbele ya bondia wa Jamhuri ya Moldova, Vasilii Belous.
Kidunda ametolewa katika raundi ya kwanza kabisa kwa kuambuliwa pointi 7 – 20 dalili inayoonesha kuwa bondia huyo hakuwa na maandalizi ya kutosha.
Kutokana na kuelemewa kulikoonekana wazi kwa bondia huyo wa kitanzania, majaji watano wa pambano hilo walimpa ushindi mmoldova huyo ambaye ni mdogo kiumri kwa Kidunda.
Katika michuano ya Olimpiki 2012 jijini London, Tanzania inawakilishwa na wanamichezo sita ambapo matokeo hayo ya Kidunda yanamaanisha kuwa matumaini ya Tanzania kupata medani yamebaki kwa wachezaji watano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents