Habari

Tanzania yanyemelewa na gonjwa jingine

WANAUME wanaowaingilia wanyama au kupenda kufanya mapenzi na wanawake wanaowazidi sana umri, wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia ambayo tiba yake ni ushauri.

Basil Msongo


WANAUME wanaowaingilia wanyama au kupenda kufanya mapenzi na wanawake wanaowazidi sana umri, wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia ambayo tiba yake ni ushauri.


Daktari bingwa wa magonjwa ya akili nchini, Profesa Gad Kilonzo aliiambia HabariLeo Jumapili kuwa tatizo hilo huwakumba pia wanawake wanaopenda kufanya mapenzi na vijana wadogo wa kiume. Alilitaja tatizo hilo kitaalamu kuwa ni Zoophilia. Alisema watu wenye kupenda kufanya vitendo vya namna hiyo wanakuwa na tatizo sehemu ya ubongo wao ambayo inahusika zaidi na kutoa uamuzi wa busara kabla ya kutenda.


Kwa mujibu wa maelezo ya mtaalamu huyo, sehemu hiyo ya ubongo humsukuma mtu kuwa tamaa ya kufanya hivyo baada ya kuwa imeharibika kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo kuingiliwa na sumu kutoka mwilini au kwenye mazingira, unyanyasaji, au mtu akiumia kichwani. Alisema, Zoophilia ni miongoni mwa matatizo ya kisaikolojia yanayohusiana na masuala ya kujamiiana, likiwamo tatizo la wanaume wanaosikia raha kufanya mapenzi hata na maiti. Prof. Kilonzo alitaja tatizo jingine kuwa ni Voyeurism linalowakumba wanaume wanaopenda kujificha mahali ili kuwachungulia wanaovaa au kuvua nguo.


Kwa mujibu wa maelezo ya mtaalamu huyo wa magonjwa ya akili katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili jijini Dar es Salaam, wanaume wengine hujisikia raha wanapojamiiana na watoto wa kike ambao hawajavunja ungo. Alitaja tatizo jingine miongoni mwa hayo kuwa ni lile la wanaume wanaojisikia raha na hata kumaliza haja zao kwa kuwaonyesha wanawake uume wao na wanaume wanaopata ridhiko kwa kugusana tu na wanawake bila kuwaingilia au wale wanaoridhika baada ya kupigwa sehemu mbalimbali za mwili.


Alisema matatizo hayo, yanayoweza kuwa ya kudumu huwakumba pia wanawake wakiwamo wanaojisikia raha kujamiiana na wavulana au wanaume wenye umri mdogo kuliko wao. Prof. Kilonzo alisema, matatizo hayo husababishwa na mambo mbalimbali wakati wa ukuaji wa mhusika, ikiwa ni pamoja na kukosa fursa za kuwa na mahusiano na makundi mbalimbali, wakiwamo watu wa rika lake, jamii inayomzunguka au watu wa jinsia tofauti.


Alisema, tiba ya matatizo hayo si dawa za kumeza au sindano, ni msaada wa kisaikolojia anaopewa mhusika baada ya kueleza historia ya maisha yake, mazingira anayoishi, sehemu alizopitia, watu wanaoishi nao na mambo mengine yanayomhusu.


Prof. Kilonzo alisema, msaada huo huanza kuleta mabadiliko kuanzia miezi sita na kuendelea baada ya mhusika kuanza kushirikiana na wenzake kwenye mambo mbalimbali, wakiwamo wa jinsia tofauti na pia kushiriki michezo.


Kwa mujibu wa kifungu cha 154 cha Kanuni za Adhabu za Tanzania, mtu akikutwa anafanya hivyo anastahili adhabu ya kifungo cha maisha au kifungo kisichopungua miaka 30 jela.


Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents