Tia Kitu. Pata Vituuz!

Tanzania yaongoza Afrika kuwa na idadi kubwa ya vijiji vyenye Umeme, Waziri athibitisha hilo – Video

Tanzania yaongoza Afrika kuwa na idadi kubwa ya vijiji vyenye Umeme, Waziri athibitisha hilo - Video

Kupitia kwa maelezoa ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameeleza na kufafanua kwa kupitia mradi wa Umeme vijijini REA.

Waziri ameeleza kuwa mpaka hivi sasa vijiji vilivyopitia na kupata huduma ya Umeme ni zaidi ya vijiji 9001 kutoka vijiji 2018 ambavyo vilikuwa na umeme mnamo mwaka 2015.

Waziri ameongeza kwa kipindi hiki cha miaka minne takribani vijiji 7000 vimepatiwa huduma ya Umeme, Idadi hiyo inakamilisha asilimia 75 nchi nzima kwa vijiji vilivyopatiwa Umeme.

Kiwango hicho kinaifanya nchi yetu kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na idadi kubwa ya vijiji vilivyopitiwa na Umeme huku ikifuatiwa na Nigeria.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW