Michezo

Tanzania yapanda kwa nafasi 2 kwenye viwango vya FIFA, sasa ni ya 118

Tanzania imepanda kwa nafasi 2 kwenye viwango vipya vya FIFA na kukamata nafasi ya 118. Viwango hivyo vya FIFA vimetoka leo, Alhamis ambapo Tanzania imepata pointi 261.

fifa

Hata hivyo hakuna mabadiliko makubwa kwenye viwango hivi vya January kwakuwa hakuna mechi nyingi zilizochezwa mwenzi December. Hispania bado imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani. Hispania imepata pointi 1,507 ikifuatiwa na Ujerumani (1,318) na Argentina (1,251).

Brazil wamebaki katika nafasi ya 10 huku Ivory Coast ikiwa nchi ya Afrika iliyoshika nafasi ya juu, 17. Viwango vijavyo vitatangazwa February 13.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents