Michezo

Tanzania Yapanda viwango FIFA

 

Tanzania imepanda hatua moja kwenye viwango vya ubora wa soka inayotolewa


na shirikisho la soka la kimataifa. FIFA Ikiwa siku chache baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Kenya.

Tanzania ambayo timu yake ya taifa juzi Jumatano iliumana na Harambee Stars ya Kenya kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam,imepanda kutoka nafasi ya 112 mpaka ile ya 111, sambamba na Rwanda wakiwa wamelingana kwa point 235.

Wakati Tanzania timu yake ya taifa inayofundishwa na Jan Poulsen raia wa Denmark ikipanda majirani zetu Kenya wameshuka nafasi moja chini na kuwa 116,huku Uganda ikpanda nafasi moja na kuwa ya 69.

Katika msimamo huu timu 13 za juu hazijabadilika kutokana na kuendelea kuwa kwenye nafasi zao za awali huku Hispania ikiongoza ikifuatiwa na Uholanzi na Brazil. Misri imeendelea kuongoza kweye msimamo huo wa upande wa Afrika kwa kushika nafasi ya 9 ikifuatiwa na Ghana nafasi ya 23,Ivory Coast 26 wakati Nigeria 30 na Algeria 33.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents