Michezo
Tanzania yapanda viwango vya FIFA wakati Uganda haikamatiki Afrika Mashariki, Ubelgiji yaongoza
Tanzania imefanikiwa kupanda kwenye viwango vya soka duniani kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa miguu duniani (FIFA) kutoka nafasi ya 140 mpaka 136.
Katika viwango hivyo vilivyotolewa hii leo siku ya Akhamisi ya Oktoba 25, 2018 Tanzania imepanda kwa nafasi nne kutoka hiyo ya 140 mpaka 136.
Kutazama viwango vyote vya FIFA A-Z bofya hapa
Kwenye viwango hivyo Uganda wameendelea kuongoza ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa kushika nafasi 79 wakipanda nafasi nne wakati Kenya ikishika nafasi ya 105 nao wakipanda kwa nafasi mbili.
Nchi zinazoongoza kwenye viwango hivyo | |
---|---|
1. | Belgium |
2. | France |
3. | Brazil |
4. | Croatia |
5. | England |
6. | Uruguay |
7. | Portugal |
8. | Switzerland |
9. | Spain |
10. | Denmark |
18. | Wales |
33. | Republic of Ireland |
34. | Northern Ireland |
40. | Scotland |