Tupo Nawe

Tanzania yapokea vifaa tiba vya Bilionea Jack Ma, kupambana na virusi vya corona

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tayari Tanzania imepokea msaada wa shehena ya vifaa tiba kutoka kwa moja ya wafanyabiashara maarufu nchini China Jack Ma. Vifaa hivyo viliwasili jana usiku na ndege ya shirika la Ethiopia.

 

Katika taarifa yake aliyoiandika kupitia ukurasa wake wa  Twitter Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, amemshukuru mfanyabiashara huyo pamoja na Serikali ya China kwa ujumla.

“Jana usiku sisi Tanzania tulipokea mchango wa vifaa tiba, ambavyo vitasaidia katika mapambano yetu dhidi ya COVID-19, shukrani zetu za dhati kwa mfanyabiashara JackMa na taasisi yake ya AlibabaGroup na Serikali ya Ethiopia” Ameandika Waziri Ummy.

Kupitia Alibaba Foundation na Jack Ma Foundation imetoa msaada wa baroka (maski), vifaa vya kupimia virusi vya corona na ‘suits’ za kujilinda, kwa nchi za Afrika katika jitihada za kupambana na  janga hilo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW