Tupo Nawe

Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake utakua kwa kasi kufikia 2026

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha utafiti wa maendeleo (Harvard’s Center for International Development) wa chuo kikuu cha Harvard nchini Marekani, kimeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya 4 kwa kasi ya ukuaji wa uchumi hadi hadi kufikia mwaka 2026.

Tanzania ipo nafasi ya nne ikiwa ambayo inakdiriwa kwa ukuaji wa 6.15% nyuma ya India 7.9%, Uganda 7.4% na Misri 6.6%, ambapo nafasi ya tano imeshikiliwa na Indonesia, Kyrgyzstan, Pakistan, Vietnam,  Mali na Kenya inashika mkia kwenye nafasi ya 10.

Hata hivyo, ripoti hiyo imezitaja nchi za India na Indonesia kuwa ni nchi ambazo zitakua kwa kasi zaidi kiuchumi duniani kwa miaka 10 ijayo.

Utafiti huo unaonesha kuwa ukuaji wa uchumi barani Afrika unaanza kuhama kutoka Afrika Magharibi ambako nchi nyingi zimeonekana kudumaa na kuhamia Afrika Mashariki.

Sababu za nchi nyingi za Afrika  Mashariki kuonekana uchumi wake kukua kwa kasi ni uuzaji wa malighafi nje ya nchi na utekelezwaji wa sera za viwanda hii ni kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Soma zaidi ripoti hiyo kwa kubonyeza link ifuatayo-Southeast Asia Surging in CID’s New Global Growth Projections

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW