Tupo Nawe

Tanzania yazindua ATM ya kwanza ya maziwa (+Picha)

ATM ya kwanza inayotoa maziwa imezinduliwa jana Oktoba 3, 2019 kwa mara ya kwanza mjini Moshi mkoani Kilimanjaro yenye uwezo wa kutoa maziwa kulingana na kiwango cha fedha yako.

Mashine hiyo imefunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira katika mji wa Moshi mtaa wa chaga karibu na soko la kati.

Hii inakuwa ATM ya kwanza ya maziwa kuzinduliwa Tanzania.

ATM hii ina uwezo wa kutoa maziwa kulingana na kiwango chako cha fedha. Unaweza pata kuanzia Tsh. 100, 400, 600, 1000, 2000, na kuendelea.

Mradi wa ATM hizo, umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na kwa kuanzia wameweka ATM tatu katika wilaya ya Moshi, Hai na Arusha Mjini.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW