Habari

Tanzania’s Next Top Model kusakwa

 

Shindano la kumsaka Mwanamitindo bora wa Tanzania, ‘Tanzania Next Top Model’, lililokuwa lifanyike Novemba 27 sasa limepangwa kufanyika Desemba 3 mwaka huu katika  kwenye Ukumbi wa Sweet Easy jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Smilling Faces Caroline Zayumba  ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo, alisema hayo  jijini Dar es Salaam jana,   kuwa wamesogeza mbele shindano hilo ili washiriki wengi wahudhuria katika mahafali ya kuhitimu elimu zao katika ngazi ya vyuo vikuu, ambako  kwa kipindi  hicho hawatakuwa katika majukumu hayo.

Carolina  aliendelea kusema kuwa  kutokana na sababu hiyo iliyotolewa na washiriki wengi, tumeona ni bora kuahirisha shindano hadi katika muda huo uliopangwa.

Baadhi ya washiriki katika shindano hilo, tayari wameishaanza kuchujwa na mmoja wa majaji wa shindano hilo Nafsika Calviaris, kutoka nchini Marekani kutokana na kushindwa kufikia vigezo vinavyohitajika na waandaaji.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents